Itagharimu nini

Yesu alikuja duniani kama Mungu katika mwili kushughulikia shida zetu kuu mbili.kwa kifo chake msalabani alitulipia gharama ya dhambi zetu,kwa hivyo akashughulikia shida ya DHAMBI alipotoka kaburini akiwa mzima siku ya tatu alikuwa na ushindi juu ya kifo na kaburi kwa hivyo akashughulikia shida ya KABURI. Na ulisoma kuwa ili uunganike na INJILI lazima mmoja awe na haja ya kubatizwa katika kifo chake ,katika maji, katika damu yake. Lakini kabla uchukue hio hatua ya mwisho lazima utambue gharama.Wokovu ni bure. Yani Yesu alitulipia gharama, Lakini tunapofanya uamuzi wa kufanyika wakristo,mmoja atatezwa kwa ajili ya imani.Yesu aliwambia wanafunzi wake kuwa isiwashangaze.

Soma kile Yesu alisema katika Yohana15:20″Likumbukeni lile neno nililowambia,mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake, ikiwa waliniudhi mimi,watawaudhi ninyi,ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu.” Kama walimwudhi Yesu watawaudhi ninyi mnapofwata injili.Yesu aliendelea kufundisha jinsi mateso haya yanaweza kuwa mengi.Hata ikatoka kwa familia ya mtu mwenyewe.Lakini vile Yesu alifundisha mtu inafaa awe na moyo wa kuangazia gharama.

Soma Luka14:26-28 kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake na mama yake,na mkewe,na wanawe,na nduguze, waume na wake,naam na hata nafsi yake mwenyewe hawezi kuwa mwanafunzi wangu.Mtu yeyote asiyechukua msalaba wake na kunifwata hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Maana ni nani katika ninyi kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kukamilisha?Kuhesabu gharama inahitajika kujitolea.

Soma maneno ya mtume petero katika 2petero2:20-21 kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo kama wakinaswa tena na kushindwa hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ya kwanza, kwa kuwa ingekuwa heri kwao kama wasingalijua njia ya haki kuliko kuijua kisha kuiwacha ile amri takatifu waliopewa. Mtu anaitii injili inatufaa kushinda majaribu ambayo yanaweza kuja mbele zetu. Hii inahitajika kujitolea kabisa.kama uko tayari kuchukua hatua inayofwatia, soma kifungu kifwatacho kwa sauti na kisha umruhusu Mungu ajue jawabu lako .

Matendo ya mitume22:16 Basi sasa unakawia nini? Simama,ubatizwe,ukaoshwe dhambi zako, ukilitia Jina la Yesu: Kama uko tayari kubatizwa tafuta mtu ambaye atakupeleka mtoni,kisimani,ama mahali popote palipo na maji mengi na umruhusu akuzamishe(akubatize) katika Kristo kwa msamaha wa dhambi(ondoleo la dhambi) na kupokea Roho Mtakatifu. Tafadhali usikawie ni swala la UZIMA na KIFO. Uzima wa milele umo.Kama uko na kanisa la Kristo ama kanisa la Kikristo karibu nawe enda uulize mshirika wao akubatize. Sisi katika huduma ya kurai urejesho na huduma ya Linda ( kulea) twaomba kwamba utatii INJILI na uzikwe(ubatizwe) katika kifo cha Kristo. Mungu awabariki , na wacha apokee Utukufu WOTE. Kama umeitii injili tutafurahi kusikia kutoka kwako ! Ama kama swali lolote, twaweza kusaidia kupata majibu kutoka katika maandiko.

Wasiliana nasi !