Yesu ni nani

Tunaanza na swali lililoulizwa hapo awali :

Uhusiano wako na Mungu unaendeleaje? Ikiwa Bwana angerudi Leo, unajua kwa UHAKIKA bila shaka, kuwa unaweza kuishi naye Milele ?Unajua kwa UHAKIKA kuwa unaenda mbinguni? Na hata mtu anaweza jua?

Kuna HABARI NJEMA! Kama vile maandiko inafundisha, mtu anaweza jua! Na hio kweli ni HABARI NJEMA. Sasa Kama uko na biblia, fwata vile habari njema, na kutii injili na unaweza kuwa na uhakika na uzima wa Milele.Kama uko tayari bonyeza hapa chini kuanza uasilishaji injili ambao utakupa habari njema nzuri utakayokuwa ukiisikia milele

Sasa Kama uko na biblia, enda kwa agano jipya. Yohana wa kwanza 5:13 .Mtume Yohana anaandika kuwa tunajua jinsi ya kupata uzima wa milele. Aliandika :Vitu hivi nawaandikia mnaoamini jina la mwana wa Mungu, ili mweze kujua kuwa mna uzima wa Milele .Lakini inafaa kujiuliza iliyoandikwa katika biblia kuhusu UZIMA na MAUTI(Kifo) .Unahitajika kuwa makini Sana biblia inaposema kuhusu UZIMA(uzima wa Milele, umilele,mbinguni,wokovu)na MAUTI(hukumu,ghadhabu ya milele, kutengwa na Mungu)

Soma iliyoandikwa, Ikinukuu maneno ya Yesu katika Yohana8:24″sasa niliwaambia mtakufa katika dhambi zenu,msiponiamini,mtakufa katika dhambi zenu “Habari njema ni:-Yesu anasema hatustahili kufa katika dhambi zetu. Yesu anasema tuamini kuwa “Mimi ndimi ” Hili huturejesha katika swali,YESU NI NANI? “Mimi ndimi”

Yesu siku moja akauliza wanafunzi wake swali hili. Hivi ndivyo ilivyorekodiwa katika Mathayo 16:13-17

Wakati Yesu alikuja katika mji wa kaiseria ya Filipi, alikuwa anauliza wanafunzi wake “watu wanasema Mimi ni Nani? ” Na wakasema baadhi Yohana mbatizaji, wengine Eliya,lakini wengine Yeremia au mmoja wa manabii :Akasema nanyi mnasema Mimi ni Nani? Simeoni Petero akajibu”wewe ni Kristo, mwana wa Mungu aliye Hai” Yesu akawambia, “umebarikiwa wewe simoni kwa sababu mwili na damu haijakuvunulia lakini ni baba aliye mbinguni.

Tambua katika mistari hapo juu ya mathayo simoni Petero akajibu, “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai Neno Kristo humaanisha “mpakwa mafuta ” Yule aliyeteuliwa kwa makusudi. ” Agano la kale liliandikwa katika lugha ya Kiebrania linatumia neno “Masiya ” Yesu ndiye atakayetimiliza unabii wa agano la kale kuhusu Masiya. Petro anasema anayofanya hayo ni Yesu .Petro pia anaongezea “mwana wa Mungu aishiye milele ” Lakini ni mwana wa Nani? Yesu atatujibu hiyo mwishoni mwa kifungu cha Mathayo “Babangu aliye mbinguni “Lakini anaamini kuwa Yesu ni Kristo, mwana wa Mungu aliye hai, yote tunahitajika kuamini kuhusu kutambulika kwake?

Wacha tuendelee kusoma bibilia na kuendelea kujibu maswali yetu. Tambua hii unaposoma Yohana 1:1 vile inasema. “Hapo mwanzo kulikuwako neno, naye neno alikuwa na Mungu, naye neno alikuwa Mungu.

Yesu anapokuwa mwana wa Mungu, ni Mungu. Angalia jinsi mtume Yohana anaendelea katika Yohana 1:14. “Na neno likafanyika mwili, na kukaa ndani mwetu, na tukaona utukufu wake, utukufu uliotoka kwa Mungu wa pekee aliyejawa na Neema na Ukweli “

Yesu alipokuja duniani, ama Kama vile Yohana alivyoandika. “Ikafanyika mwili” Je ,Yesu alijawa uungu mbinguni? Tambua unaposema Wakolosai 2:9 kufwatia Yesu ni asilimia 100 o/o mtu na asilimia 100 o/o Mungu. Ju katika yeye ukuu na utimilivu wote upo katika mfano wa mwili.

Wakati mtume Paulo aliandika ujumbe huo katika Wakolosai, “Katika yeye “alikuwa anasungumzia Yesu. Ukamilivu wa ukuu wote (ambao ni jinsi ya Mungu alivyo) katika mwili (mwili wa mwanadamu) mfano! Yesu alikuwa Mungu katika mfano wa mwanadamu. Sasa tambua kwamba Mungu baba anamwita mwanawe. Hivi ndivo mwandishi wa kitabu cha waebrania vile anaiweka Waebrania1:8. Lakini kwa mwana anasema, “KITI CHAKO CHA ENZI, EE MUNGU, NI CHA MILELE. “Mmoja auliza, ingawa, Kumbe Yesu alisema yeye ni Nani? Je, Yesu alisema yeye ni Mungu katika mwili?

Tambua hii katika Yohana 8:58 ya kwamba Yesu alisema kuwa yeye ni “ndiye aliye “Yesu akawambia “amini ! Amini ! Nawambia kabla Ibrahimu azaliwe. “ndiye aliye “Ndio ujue kuwa unao uzima wa milele (usemi wa UZIMA) na usife katika dhambi zako (Usemi wa kifo) Inafaa kuamini kuwa Yesu ndiye bibilia inasema “ndiye aliye “Lazima tuamini kuwa Yesu ni Mungu. Ama tunakufa katika dhambi zetu. Bibilia inatufundisha kuwa kuna utatu katika uungu.

Soma jinsi Mathayo 3:16-17 hutaja Mungu baba, Mungu mwana, na Mungu Roho mtakatifu. Tatu katika moja. Baada ya kubatizwa Yesu alitoka majini na papohapo tazama mbingu ikafunguka na akaona Roho wa Mungu akishuka mfano wa njiwa na mwanga Mkubwa juu yake, na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema “Huyu ni mwanangu nimependezwa naye “Tambua Mungu baba -sauti kutoka mbinguni ,Mungu mwana -mwanangu mpendwa, Mungu Roho mtakatifu -Roho wa Mungu. Yesu ndiye wa tatu katika uungu.

Lakini Yesu alifanyaje na kwa nini alifanya? Bonyeza hapa chini na uendelee.

onyeza kwenye picha hapo juu kuendelea na masomo