Nawezaje Kuingia Katika Injili

Yesu Mungu katika mwili alikuja duniani na akafa kwa ajili ya dhambi zangu.kifo chake kilishughulikia dhambi zetu.Hakuishi kaburini bali alifufuka siku ya tatu.kupitia kwa kufufuka kwake alishughulikia shida yetu ya KABURI.Lakini ni vema tujue jinsi ya kuingia katika injili hii. Tunarudia baadhi ya usemi wa UZIMA na KIFO tunapata katika maandiko.Unaposoma Warumi 10:9 Tambua kile ambacho tunahitajika kukifanya ili tuokoke.Kiri na kinywa chako kuwa Yesu ni Bwana,na kuamini moyoni mwako kuwa alimfufua katika wafu,utaokoka.

Mtume Paulo aliyeandika kitabu cha warumi anatwambia kuwa tunahitajika kwa LAZIMA kufanya vitu viwili:

1.Kiri Yesu ni Bwana
2.Amini kuwa alimfufua katika wafu.

Sasa katika usemi huu wa UZIMA na KIFO tunasoma kuwa, kama tunataka kuokoka lazima tukiri na lazima tuamini injili.Bibilia pia inatwambia kuwa LAZIMA tubadilishe maisha yetu.Kuna mistari mingi katika bibilia inayofundisha haya lakini wacha tusome chache ili tuone ni mabadiliko yapi tunahitajika kufanya. Soma 1 Wakorintho 6:9-10 na utambue mabadiliko ya maana lazima yafaa tuyafanye. Ama hujafahamu kuwa wasio haki hawataridhi ufalme wa Mungu? Usidanganywe,waesharati,waabuduo sanamu,wazinzi,wafiraji,walawiti,wezi,watukanao,wanyang’anyi hawatauridhi ufalme wa Mungu.Vitabu vingine ambavyo vinaweza kusomwa ni Waefeso 4:17-5:7 ,Wagalatia 5:19-26,Warumi 1:28-32 Ili kuridhi ufalme wa Mungu, kuokoka kuna mabadiliko lazima tuyafanye. Bibilia inayaita kutubu.Lakini nini kinatendeka tunapoamua kubadilika? Ama tuamue kutobadilika? Nini kitatendeka? Soma yale Yesu anasema katika Luka 13:3,5

“Nawambia la hasha ,lakini msipotubu,pia nanyi mtaangamia”

Tambua kuwa Yesu anatumia maneno UZIMA na KIFO. Tukiamua kutobadilika ,tutaangamia. Sasa tukitaka kuingia katika neema ya Mungu iokoayo inafaa tufanyaje? Mtu anawezaje kuingia katika injili?Soma maneno ya mtume Paulo katika 2 Wathesolonike 1:7-9

Na kuwalipa ninyi mtwezao raha pamoja na sisi.wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake. Katika mwali wa moto, huku akiwalipisa kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasiotii injili ya Bwana wetu Yesu.watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele,kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.

Nawezaje kuhepa hukumu ya Mungu- moto uwakao ,kisasi,maangamizo ya milele mbali na uwepo wa Bwana? Kulingana na maandiko lazima tutii injili ya Bwana wetu Yesu. Lakini mtu awezaje kuamini injili? Soma vifungu vifwatavyo na utaona injili ikidhihirishwa pale.Unakumbuka injili ni nini? Kufa ,kuzikwa na kufufuka kwa Yesu. Hapa kuna Warumi 6:3-6

Hamkufahamu ya kuwa sisi sote tulibatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa baba ,vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake mkijua neno hili kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye ili mwili wa dhambi ubadilike tusitumikie dhambi tena .

Tunawezeje kujiunganisha na kifo cha Yesu?Bibilia inasema tunabatizwa katika kifo chake.Mtu huzikwa pamoja na Kristo na kufufuliwa kutembea katika upya wa uhai.Kisha soma Warumi 6:17-18

Lakini Mungu ashukuriwe maana mlikuwa watumwa wa dhambi,lakini mlitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake.na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi mkawa watumwa wa haki.Lakini kwa nini

Mungu aturuhusu tuhusishwe katika kifo cha Yesu? Pengine picha hii inawezaonyesha mtu ambaye anatii injili na kujibu swali hilo.

Bonyeza kwa picja ili uione kikamilifu.

Sasa ni wapi hakika mtu anaweza kufanyika mkristo? Wagalatia 3:26-27 hujibu swali hilo.Kwa kuwa wote ni wana wa Mungu kupitia kwa imani katika Kristo Yesu.kwa kuwa ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.

onyeza kwenye picha hapo juu kuendelea na masomo